Do you have any Question?

Do you need an assistance? or you what to ask more about our safari packages? here is our number to call directly to our office

255 677 113 333
Safari ya kibishara kwenda DUBAI, UAE 9 - 13 Dec 2020

Safari ya kibishara kwenda DUBAI, UAE 9 - 13 Dec 2020 - Price start from 2000$


Dubai kama kitovu cha Biashara hasa likiwa kama Soko la Dunia kwa kununua na kuuza bidhaa mbali mbali kutoka nje na ndani ya Nchi yao, Aidha Dubai ni kati ya Nchi zenye fursa nyingi za Kibiashara kwa kuwa na milango wazi kwa watu wa mataifa yote kufungua Biashara Nchini Dubai kwa gharama nafuu mno, Pia Nchini Tanzania, Makampuni mengi ya kitanzania
yanafanya biashara na Dubai kwa kiasi kikubwa ingawa wanakutana na changamoto mbalimbali za kibishara ikiwemo upatikanaji wa wadau sahihi wa kufanya nao biashara, upatikanaji wa malighafi kutoka kwa makampuni ambayo yana zingatia ubora wa bidhaa n.k hivyo basi Go Etra Mile Safaris wameandaa safari hii ya kibiashara na kimafunzo zaidi ili kuwajengea
watanzania uwelewa mkubwa wa namna ya kufanya biashara na Dubai.

Safari hii ya kibiashwa itakuwa na mambo makubwa matatu:-

  • Kutembelea Masoko pamoja na Taasisi mbalimbali za Kiserikali, Binafsi na Wadau wa Biashara,
  • Kuhudhuria kongamano la kibiashara kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Dubai
  • Kutembelea Viwanda na Makampuni mbali mbali kulingana na Sekta yako ikiwa ni pamoja na elimu ya jinsi yakufungua biashara Nchini Dubai

Madhumuni ya safari hii ya kibiashara ni kuwasaidia washiriki; Kupata fursa ya kuanzisha ushirikiano wa biashara, Kupata ujuzi wa Teknolojia mbalimbali na juu ya jinsi ya kuanzisha viwanda, Kupata nafasi ya kufanya majadiliano ya biashara na kupromoti bidhaa za kitanzania kwenda Dubai mfano mazao yetu ya kilimo, madini, Ngozi, viungo n.k.

Sekta muhimu kwa Safari hii: Agro Processing Machineries, General Machinery, Small Processing Machinery, Construction Equipment, Vehicles & Motorcycles Spare Parts, Electronics & Household Electrical Appliances, Lighting Equipment, Hardware & Tools, Energy + Resources, Chemical Products, Building Materials, Agriculture equipments, Mining Industry, Cloth Industry, Printing and Stationaries etc.

Baraza la Biashara kati ya Dubai na Tanzania huko Dubai, UAE.

Kwa kushirikiana na Taasisi mbali mbali za kiserikali na zisizo za kiserikali za Nchi za Kiarabu, tumeandaa kongamano la biashara kati ya Dubai na Tanzania kwa ajili ya wafanyabiashara watakaokwenda katika ziara hii kwa kusudi la kutoa nafasi kwa nchi yetu Tanzania kuhamasisha uwekezaji hapa nchini na pia kutoa fursa kwa wafanyabiashara kupata nafasi ya kupata
wabia wa kushirikiana kuwekeza na kuanzisha viwanda hapa nchini pamoja na kupanua wigo wa biashara yako kwa kuweza kuwa na Tawi Nchini Dubai na kupata Masoko ya bidhaa zetu katika nchi za Arabuni, Kongamano hili litatoa fursa kamili ya kukutana, kufahamiana, kujadili na kuanzisha ushirikiano na wenzao wa Kiarabu kupitia mkutano wa B2B.

Included

  • ​Flight ticket
  • Hotel and city tour
  • Business forum
  • Visa and travel insurance

Excluded

  • Personal expense
Book this safari now:
Full name
Your country
Email address
Phone number
How many are you
Check in
Check out